Tuesday, April 30, 2013

PADRI AKAMATWA AKIVUNJA AMRI SITA MKE WA MTU HUKO MOSHI

KANISA Katoliki Jimbo la Moshi
limeingia katika kashfa nzito baada
ya padri wake, Father Urbanus Ngowi
wa moja ya parokia zake kudaiwa
kufumaniwa na mwanamke
anayesemekana ni mke wa mtu,
Ijumaa Wikienda lina sakata zima.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa
kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita
chumbani kwa padri huyo, Marangu
Wilaya ya Moshi Vijijini ambako
Father Ngowi inasemekana alikutwa
‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo
aliyejulikana kwa jina la kijamii la
Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo
havijaeleza humo chumbani wawili
hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio,
mwanamke huyo aliingia nyumbani
kwa padri huyo ambapo baadhi ya
ndugu wa mumewe walikuwa
wakimfuatilia baada ya madai
yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu
wenye maswali mengi na mtumishi
huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba
Mama P na Father Ngowi wana
ukaribu wenye maswali mengi, mume
wake alifuatilia na kubaini ni kweli
lakini akashindwa kuutenganisha
ukaribu wao,” kilidai chanzo.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba
baada ya kuona mkewe amejikita kwa
mtumishi wa Mungu, mumewe (jina
tunalo) alinyoosha mikono juu na
kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya
ndugu wa mume kumfuatilia mpaka
anaingia kwa Father Ngowi, wakaona
ni bora watafute mpigapicha ili
kupata picha za tukio ambazo
zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani,
sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta
mwanamke huyo na mtumishi wa
Mungu wapo kitandani.”
AWEKWA KITIMOTO
Habari zinadai kwamba kufuatia
tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki
limemweka kitimoto padri huyo
ambaye alikuwa akihudumu katika
Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini
kabla ya kuhamishwa na kupelekwa
Parokia ya Makomu, Marangu ambako
inadaiwa ameshushwa cheo.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo,
Father Ngowi alikana kukutwa na
mke wa mtu chumbani kwake lakini
alipobanwa sana na mabosi wa
Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi,
alikiri na kudai ibilisi alimpitia na
kuomba kanisa limsamehe na
kutompa adhabu kali ambayo
itamuathiri kisaikolojia.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake
kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki
nchini kwa padri wake kudaiwa
kukutwa na mke wa mtu chumbani
kwake!
SIKU ZA NYUMA
Kuna madai kwamba mwaka jana
(2012), Father Ngowi, mbele ya
waumini wake alisoma barua yenye
kukana shutuma zote zilizoelekezwa
kwake kwamba amekuwa na ukaribu
wenye maswali mengi na wake za
watu.
Taarifa zilidai kuwa padri huyo
aliweka wazi akisema si kweli
kwamba amekuwa na ukaribu
unaotajwa, akawataka waumini wake
wapuuze tuhuma hizo alizosema zina
mwelekeo wa kuchafua sifa yake na
taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.
Hayo ni madai ya vyanzo vyetu
ambavyo viliambatanisha na picha
mbalimbali za tukio hilo lenye
kushtua waumini sambamba na
namba za simu za padri huyo kwa
ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
IJUMAA WIKIENDA NA FATHER
NGOWI SASA
Baada ya kujazwa madai hayo, kama
ilivyo desturi ya Magazeti ya Global
Publishers likiwemo hili (Ijumaa
Wikienda), lilimsaka Father Ngowi
kwa udi na uvumba ambapo Ijumaa
iliyopita nyakati za mchana
lilifanikiwa kuzungumza naye lakini
kabla ya kufanya hivyo, kifaa cha
kunasia sauti kiliwekwa sawa na
mambo yalikuwa hivi:
Wikienda: Haloo, naongea na Father
Ngowi wa Parokia ya Korongoni,
Marangu, Moshi?
Father Ngowi: Naam ni mimi, nani
mwenzangu?
Wikienda: Naitwa…(mhariri anataja
jina), napiga simu kutoka Magazeti
ya Global Publishers.
Father Ngowi: Uko wapi?
Wikienda: Makao Makuu ya Global
Publishers, Dar es Salaam.
Father Ngowi: Eeh…unasemaje?
Wikienda: Kuna madai ya wewe
kukutwa na mke wa mtu chumbani.
Je, unaweza kunielezea kama ni
kweli na tukio lilikuwaje?
Father Ngowi: Siyo mimi.
Wikienda: Wewe siyo Father Urbanus
Ngowi?
Father Ngowi: Nimekwambia siyo
mimi, hao ni matapeli wanataka pesa
ndiyo wametengeneza hizo picha.
Wikienda: Kwa hiyo unataka
kuniambia hizi picha ni za
kutengeneza?
Father Ngowi: Nimekwambia hao ni
matapeli wanataka pesa.
Wikienda: Ulishaziona picha
zenyewe?
Father Ngowi: Sijui.
NGOMA YATUPWA KWA MKUU WA
JIMBO
Wikienda: Mbona tayari tukio hilo
linadaiwa limeshafika kwenye ngazi
ya jimbo, Moshi kwa Father Paul
Uria?
Father Ngowi: Muulize yeye ndiye
mkubwa wangu.
Wikienda: Basi nisaidie namba yake
ya simu ya mkononi.
Baada ya takribani dakika 10, Father
Ngowi alituma namba ya simu ya
Father Uria na mambo yakawa hivi:
Wikienda (huku kinasa sauti
kikiendelea kufanya kazi): Haloo…
naitwa …(mhariri anajitambulisha)
kutoka Magazeti ya Global
Publishers, Dar es Salaam, naongea
na Mkuu wa Jimbo Kanisa Katoliki,
Moshi, Father Uria?
Father Uria (kwa sauti yenye
unyenyekevu): Ndiyo.
Wikienda: Una taarifa za mtumishi
wako, Father Ngowi kunaswa na mke
wa mtu chumbani?
Father Uria: Kwanza mimi si mkuu
wa jimbo, ni mwakilishi wa mkuu wa
jimbo. Sipo mjini kwa sasa nipo
Kilema huku vijijini kwenye huduma
lakini nilikuta ‘missed calls’ zake
jana (Alhamisi) kwani ilikuwa
tukutane kwa sababu alishanijulisha
kuwa kuna tukio kama hilo
unaloniambia wewe.
NGOMA YAWA NZITO, YATUPWA LEO
JUMATATU
“Kweli tulikuwa tukae jana lakini
ikashindikana, leo (Ijumaa) ni
sikukuu (Muungano), kesho
(Jumamosi) na keshokutwa (Jumapili)
ni wikiendi. Kwa hiyo tutakaa
Jumatatu (leo) hivyo nipigie saa
10:00 jioni siku hiyo ili nikupe
maagizo tutakayofikia na mengine.
Wikienda: Lakini Father Ngowi
alikueleza tukio lilikuwaje?
Father Uria: Nimekwambia tukikaa
ndiyo tutajua kilichotokea. Wewe
nipigie hiyo saa 10 nikupe
kitakachojiri.
Wikienda: Shukrani Father Uria kwa
ushirikiano.
CHANZO:

No comments:

Post a Comment