
Ni wazi na dhahiri kabisa kesi
iliofunguliwa mahakamani dhidi ya
Lady JayDee haina maana yoyote
isipokuwa ni hofu ya mafisadi wa
muziki nchini (Kusaga na Ruge) kwa
kuwa waraka wa piliulikuwa utoke tar
15 may na mwingine tar 17 may
mwaka huu wa 2013.
Hapa la kujiuliza ni juu ya interview
ya Rugen a kinachoendelea sasa,eti
suala limefika mahakamani,kweli
Kusaga na Ruge mmeweza
kuthibitisha nyie ni mafisadi na
mnamuaibisha Rais Kikwete ambaye
nina uhakika anajua kuwa nyie ndio
kikwazo kikubwa na hata Bungeni
alishawahi kuzungumza kuwa alitoa
studio na pango kumbe tatizo sio
hilo,tujiulize wote kuna nini
wanachoficha hadi kumtafutia kesi
raia mwema asie na hatia?
Tena anaejitafutia rizki ambayo wao
wanapigana nayo kwa
kumkandamiza?
Huku wakitumia mabavu wakilindwa
na baadhi ya viongozi wa serikali na
waandishi ambao majina yao
mtayapata kupitia nyaraka
zinazokuja (zipo 88) na huu ndio wa
kwanza.
Nimesikitika sana na njia pekee ya
kuufahamisha umma juu ya ufisadi
huu wa Ruge Mutahaba na Joseph
Kusaga ni kuyaanika yote ambayo
jamii na Viongozi wa Serikali kama
mlikuwa hamjui sasa ndio wakati
muafaka wa kuwajua watu hawa
ambao kila kukicha ni kuimarisha
ufisadi wao na kujipendekeza kwa
Viongozi sambamba na watoto wao
(mtajua mpaka majina yao)
Naanza kupatwa na wasiwasi
nikijiuliza, endapo Lady JD angekuwa
amegombana na msanii mwenzake
mkubwa kama Prof Jay, Ray C au
Juma Nature wanasiasa wangeingilia
kati? Ni wazi wasingesogea kwa kuwa
hakuna maslahi zaidi ya kuingilia
mgogoro huu ambao hawataki jamii
ijue maovu yao.
Napatwa mashaka jinsi wanasiasa
wanavyolivalia njunga jambo binafsi
Kama hili na kulifanya ni la kiserikali
basi tafuteni chanzo cha tatizo mjue
ni sehemu gani sahihi ya kuanza
kutatua kilichopo na sio kukimbilia
kuunda vikao ambavyo naamini
vimeshaitishwa vingi sana lakini
hakuna kilichosaidia.
Wanasiasa badala ya kutafuta
sababu zinazofanya wasanii
wanalalamika mnakimbilia kutatua
mgogoro wa Ruge na JD ili
kusuluhisha mambo yasiendelee
kuongelewa jamii ijue uovu wa
mafisadi hawa.
Haitasaidia kwa sababu wanaojua
maovu ya hawa mafisadi Rugen na
Kusaga ni wasanii wengi wakubwa na
watu wengine binafsi (kumbukeni
waraka zipo 88)
Vijana mnaowategemea katika
kampeni zenu na mnawaita Taifa la
kesho, lakini mnakubali waendelee
kukandamizwa na kunyanyasika huku
wakizidi kuwaneemesha kina Ruge na
Kusaga.
Tatizo mnalijua kaeni na wasanii
wote wawaelezee matatizo yao,
msikae na wasanii ambao
wanaamrishwa na kina Ruge.
Sikilizeni kilio cha wasanii wengine
pia na itafutwe njia ya kupata maoni
ya kila mmoja na kuachana na watu
wengine ambao wanaendesha
mtandao wa ufisadi chini ya kivuli
cha Ruge (Said Fella na Babu Tale)
ambao mtapata kujua kila kitu
kuhusu ufisadi wao na
kinachoendelea (kumbuka waraka
zipo 88)
Ruge Mutahaba amekuwa ni tatizo
na janga la Kitaifa katika tasnia ya
muziki kwa ujumla, amekuwa
akiwagawa wasanii kwa kutumia
redio Clouds kwa vitisho vya
kutopigiwa nyimbo, au kwa
danganyio la kufanyiwa promotion
mpaka kwenye magazeti endapo tu
utakuwa chini ya bawa lake.
Wasanii wamekuwa hawalipwi vizuri
ili waendelee kumtegemea fisadi
huyu.
Kwani wasanii wote wangekuwa na
kipato cha kuweza kusimama imara
leo hii kauli kama ya Lady JD
ingezungumzwa karibu na kila
mwanabongoflava.
Fred Kavishe (fisadi mwingine)
ambae anasimamia Kili music awards
yuko bega kwa bega na Ruge
kudanganya wananchi nani ni bora
katika tuzo hizo ili kulinda maslahi
yao binafsi.
Na wao huchagua wale wasanii
ambao hawana sauti za kudai haki
yao ili wawatumie kadri
wanavyotaka.Tuzo za Kili ni uozo
mtupu.Imefikia wakati basata itoe
vibali kwa wadau wengine wa muziki
(nako kuna ufisadi)wasio na interest
binafsi na wasanii wao, kuendesha
hizi shughuli ili kukuza
muziki.Kutokuwepo na tuzo zingine
kunasababisha ionekane kuwa
basata nao wamo kwenye mgao wa
mabepari hao wanaoua sanaa ya
Tanzania
Location : Kisinane Rd, Moshi, Posted via Blogaway