4
P-Funk: Mangwea
alijiingiza kwenye
utumiaji wa madawa
ya kulevya kupunguza
mawazo
May 30, 2013
Producer P-Funk Majani
amefunguka na kusema kuwa
marehemu Albert Mangwea
alijiingiza kwenye utumiaji wa
madawa ya kulevya ili kupunguza
mawazo. Majani amesema kwa
muda mrefu alikuwa akijaribu
kumweka chini Mangwea
kumuonya kuhusu matumizi ya
madawa hayo lakini alikana
kuyatumia.
Ameongeza kuwa anajilaumu
kwakuwa alishindwa kufanikiwa
kumuondoa rapper huyo kwenye
matumizi ya madawa ya kulevya.
“I knew already from 2006
kulikuwa na watu wanaongeaga
kwamba anatumiaga madawa ila
kila nikimkadamiza nimweke
kwenye kiti nimwambia Ngwair
you are using ‘ohh P don’t bring
that shit you are accusing me
and I always said ‘Ngwair come
on’, amesema Majani kwenye
video aliyorekodiwa na mtandao
wa GongaMX.
“Kumbe miaka yote hiyo maskini
alikuwa anatumia. Na I look in
myself and I ask myself what is
the reason for him to do this it
was because psychologically he
was unstable. Mangwea ni mtu
ambaye amefanya vitendo
vikubwa hapa nchini lakini ile
faida na support a ukweli
hajaipata,” aliongeza.
“Ukiangalia wasanii wengine wa
Bongo Records akina Juma
Nature, Profesa Jay they got more
leverage but Mangwea was a very
big artist, he made one of the
best ever albums in Tanzania till
to date. I think that’s what drove
him slowly in depression and
people don’t use drugs unless
they are depressed. Kwasababu
mimi situation kama hiyo
ilishawahi kunifikia.”
Location : Lema Rd, Moshi,
Poudly supported by washari company
No comments:
Post a Comment