Peter Tosh (19 Oktoba
1944 – 11 Septemba 1987)
huyu alikuwa ni
mwanamuziki Mjamaika wa
mtindo wa rege, alikuwa
na kipaji mahiri cha
kutunga mashairi ya
muziki, pia alikuwa ni
mpigaji mahiri wa gitaa.
Peter alizaliwa tarehe 19
Oktoba 1944, akiwa ni
mtoto pekee wa mama
Alvera Coke, baba yake
aliitwa James Mclntosh
ambaye alikuwa ni
mhubiri wa kanisa la
Savanna-la-mar. Peter ni
jina ambalo alibadilisha
lakini jina lake halisi ni
Winston Hubert Mclntosh.
Katika maisha yake
hakubahatika kulelewa na
baba na mama yake,
alilelewa na shangazi yake
sababu wazazi wake
hawakuwa na muda wa
kumlea, hivyo huwezi
kuamini alijitunza
mwenyewe kwa baadhi ya
mambo bila kupata
matunzo kutoka kwa baba
yake ambaye alikuwa ni
baba wa watoto wengi.
Peter alianza kupiga ala
za muziki akiwa kijana wa
umri mdogo, alijifunza
kupiga kinanda kwa miezi
sita pia alijifunza kupiga
gitaa, ala hiyo ndiyo iliyo
kuja kumpa umaarufu,
mwaka 1956 baada ya
kuondoka Savanna-la-mar
Peter na shangazi yake
walikwenda mji wa
Denham katika jiji la
Kingston, Peter alipofikia
umri wa miaka kumi na
tano shangazi yake
alifariki, hivyo alikwenda
kwa mjomba wake West
Road huko Trench Town.
Peter alikutana na Robert
Nesta Marley (Bob Marley)
na Neville O'Reilly
Livingston (Bunny Wailer)
na wakajiunda kuwa
watatu wa kwanza wa
Wailer halisi na wakajiita
Wailin'Wailers, na
walianza kuimba pamoja
mwaka 1962 na alikuwa ni
yeye tu kati yao aliyeweza
kupiga ala, hivyo alifanya
bidii ya kuwafundisha
wenzake na alikuwa ni
mmojawapo
aliyemfundisha Bob
kupiga gitaa. Peter alijitoa
Wailers mwaka 1974 hii ni
baada ya Chris Blackwell
kukataa kutoa albamu yake
ya kwanza yeye akiongoza
safu ya uimbaji.
Location : Kisinane Rd, Moshi,
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment