Habari zilizoripotiwa na mtandao wa
Kenyan-Post zinasema msichana
huyo mweye miaka 23 amekuwa na
mahusiano ya muda mrefu na pasta
huyo kabla hawajabambwa.
Kisa hiki ni kama movie ambazo
tumezoea kuziona zenye story line
ambayo unaweza kutabiri mwisho
wake.
Kwa mujibu wa mtandao huo, ile
‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo
alikuwa anatarajia kusafiri kwenda
nyumbani kwao kusalimia wazazi
wake hivyo mumewe alimsindikiza
mpaka kituo cha basi, lakini
alionekana kuwa mtu mwenye haraka
na kumwambia mkewe kuwa siku
hiyo ana mkutano muhimu hivyo
anapaswa kuwahi. Baada ya
kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa
haraka na kuondoka.
Huku nyuma mke wa pasta kwa
bahati mbaya (upande wa pasta) na
bahati nzuri (upande wake)
aligundua kuwa amesahau zawadi
aliyokuwa amemnunulia mama yake
mzazi ambaye ndio anaenda
kumsalimia hivyo ikabidi airudie
nyumbani kisha asafiri na basi
litakalokuwa linafuata.
Alipofika nyumbani anapoishi na
mumewe alishangaa kukuta mlango
haujafungwa kwa nje na huku
anakumbuka walipoondoka
waliufunga hivyo akahisi huenda
wamevamiwa mchana kweupe,
alipojaribu kuusukuma ulikuwa
umefungwa kwa ndani ndipo
alipoomba msaada wa majirani
wakavunja kitasa na kuingia ndani.
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa
kile alichokikuta ndani baada ya
kumkuta msichana anayemfahamu
kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani
la mumewe wakiwa uchi wa mnyama
katika kitanda chake na mumewe.
Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia
kitandani na kuzitupa nje kupitia
dirishani nguo zao wote lakini kwa
bahati mbaya msichana
aliyemfumania alifanikiwa kukimbia
na kumuacha pasta mwenyewe.
Huwa wanasema hasira ni hasara na
maamuzi ya hasira hugeuka majuto
baadae, baada ya mmbaya wake
kukimbia aliamua kumvuta mumewe
(pasta) akisaidiwa na watu
wengine akiwa uchi wa mnyama na
kumtembeza mbele ya umati wa
watu mpaka katika kanisa analotoa
huduma pasta huyo kwa lengo la
kufichua mabaya yake.
Bahati nzuri alijitokeza mwanaume
mmoja aliempatia shati lake ili
ajisitiri.
0
Location : Lema Rd, Moshi,
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment