Kaka mkubwa wa
marehemu kusafiri leo
kuufuata mwili wa
Mangwea Africa Kusini
admin May 29th, 2013
0 Comment
Habari zilizopatikana muda huu
zinasema kuwa familia ya Mangwea
inajipanga kutuma ndugu kwenda
Africa Kusini leo (May 29) kwaajili ya
kufanya utaratibu wa kurudi na
mwili wa Marehemu Albert
Mangwea.
Akiongea na Bongo5 muda mfupi
uliopita dada wa marehemu aitwaye
Evelyn, amesema kuwa anahitajika
ndugu wa marehemu asafiri kwenda
Africa Kusini kwaajili ya kufanya
utaratibu wa kurudi na mwili,
sababu kule hawawezi kumtoa na
kumsafirisha bila ndugu yake wa
karibu kwenda.
Kwa Mujibu wa Evelyn familia iko
katika mipango ya mwisho ya safari
hiyo ambayo kaka yao mkubwa na
Mangwea ndiye anayetarajia kusafiri
leo hii (May 29) kwenda South Africa
kuufuata mwili.
“Habari mpya ni kwamba mtu atoke
hapa Tanzania aende akachukue
mwili kule hawawezi kuconfirm yaani
kumtoa kumsafirisha bila ndugu yake
wa karibu kutoka huku, kwahiyo ndio
process zinafanywa, kaka yake
mkubwa ambaye ni kaka yetu atoke
hapa aende South, ndio nadhani
atarudi na huo mwili. Ataondoka leo
hii hii muda wowote na wakati
wowote, “Alisema dada wa
marehemu Albert Mangwea.
Msiba wa rapper kipenzi cha wengi
Ngwea uko Mbezi Beach Goigi kwa
baba yake mdogo , ukishuka goigi
ukiulizia kwa mzee Mangwea kwenye
msiba utaelekezwa. R.I.P
Brother
0
Location : Lema Rd, Moshi,
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment