Tuesday, June 11, 2013

Bongo muvi yapata pigo

Marehemu Jaji Khamisi (Kashi)
Habari iliyotufikia hivi punde ni
kwamba msanii wa filamu nchini Jaji
Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na
michezo ya ITV enzi zile akiwa na
wasanii kama mzee masinde,samson
na wengine katika mchezo wa Tamu
chungu na mingine mingi Amefariki
dunia mchana huu katika hosptali ya
taifa ya muhimbili alikokuwa
amelazwa,akizungumza na the super
stars tz raisi wa shirikisho la wasanii
amesema kuwa tasnia yake bado
inaendelea kukumbwa na majanga
lakini amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee masinde ambaye alikuwa
nae katika kundi moja akiwa kama
kiongozi wake amesema kashi ni
msanii ambaye alikuwa mpiganaji na
kwa hakika ni pigo kubwa katika
tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji
Khamis (Kashi)
mahali pema pepponi Amini.

No comments:

Post a Comment