Thursday, June 13, 2013

Q the don afungua studio yake

Baada ya kufanya kazi kwa kuajiriwa
kwenye studio za watu kwa muda
mrefu, hatimaye producer wa Mchizi
Wangu ya N2N Soldier na CNN ya
marehemu Mangwair, Q The Don
amefungua studio yake mwenyewe
iitwayo, Sheidon Productions.
Studio hizo zipo jijini Mwanza
alikokaa kwa muda mrefu tangua
atokee nchini Kenya.
“Sheidon productions now
official..for them haters… tehe tehe
tehe. mungu mkubwa. patience
pays.. asante kwa wote walio amini
na kunikubali… nipo kwajili yenu…
karibuni sana,” ameandika kwenye
ukurasa wake wa Facebook.
Kwa muda mrefu Q alikuwa akifanya
kazi na studio ya MO Records ya
Mwanza na aliwahi kufanya kazi
Bongo Records

No comments:

Post a Comment