Tuesday, June 11, 2013

Kwa heri mfalme mido

Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri
Ahmed Hossam Hussein Abdulhamid
‘Mido ametangaza kustaafu kucheza
soka baada ya kucheza kwenye
kiwango cha juu kwa muda wa miaka
14 .
Mido anaweza kuwa mmoja wa
wachezaji wa Kiafrika waliowahi
kucheza soka kwenye vilabu vingi
barani ulaya akiwa amecheza kwenye
ligi za Uholanzi, Ubelgiji ,
Hispania,Ufaransa,England ,Italia na
nchini kao Misri ambapo amecheza
kwenye klabu za Zamalek alikoanzia
maisha yake ya soka wakati akiwa na
miaka 16, Gent ya Ubelgiji, Ajax
Amsterdam ya Uholanzi,Celta Vigo ya
Hispania , Olympique Marseile ya
Ufaransa,As Roma ya
Italia ,Tottenham Hotspurs ,
Middlesborough,Wigan Athletic,West
Ham United na Barnsley zote za
Engand .
Mido amewahi kuichezea timu yake
ya taifa ya Misri kwenye mechi 51
ambapo alifunga mabao 20 huku
akiwa sehemu muhimu ya kikosi
kilichotwaa ubingwa wa Afrika mwaka
2006 . Hata hivyo Mido atakumbukwa
kwa sababu mbaya kwenye timu ya
taifa yakiwemo matukio kadhaa ya
utovu wa nidhamu kama kukataa
kutolewa uwanjani na kumtolea
kocha wake Hassan Shehata maneno
machafu baada ya kutolewa uwanjani
wakati wa mchezo wa fainali ya
kombe la mataifa ya Afrika mwaka
2006 .
Mido amewahi kutwaa mataji manne
kwenye klabu za Ajax Amsterdam na
Zamalek pamoja na kombe la mataifa
ya Afrika mwaka 2006 ambapo
alifunga bao moja kwenye michuano
hiyo . Mido pia amewahi kutwaa
tuzo za mchezaji bora nchini Ubelgiji
ambako alitwaa mara mbili , tuzo ya
mchezaji bora wa Misri na tuzo ya
mchezaji bora mwenye umri mdogo
barani Afrika mwaka 2001/2002.
Mido amestaafu akiwa amecheza
jumla ya mechi 294 kwenye klabu
mbalimbali alizopita pamoja na timu
za taifa ikiwemo timu ya vijana
ambapo amefunga mabao 93 na
mpaka anamalizia safari yake ya
kucheza soka akiwa na umri wa
miaka 30 huku klabu yake ya mwisho
ikiwa Barnsley inayoshiriki ligi daraja
la kwanza nchini England ambayo
aliichezea kwenye mechi moja pek

No comments:

Post a Comment