Thursday, May 2, 2013

Baadhi ya Bodaboda Ni wez kaa chonjo

Bunduki aina ya Shortgun Mossberg
ikiwa na risasi sita ambayo ilikutwa
kwenye begi la dereva huyo wa Boda
boda aliyekamatwa na polisi tarehe
28.04.2013.
Habari na picha na Rashid Nchimbi
wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi Mkoani hapa
limemkamata mtu mmoja aitwaye
Ally Rashid Salimu (23) Mwendesha
pikipiki za abiria maarufu kwa jina la
“Boda Boda” mkazi wa kata ya
Sombetini jijini hapa akiwa na
bunduki aina ya shortgun Mossberg
yenye namba T292166 ikiwa na risasi
sita.Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake jana saa 5:30
asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Liberatus Sabas alisema
kwamba, tukio hilo lilitokea juzi
tarehe 28.04.2013 muda wa saa 3:00
asubuhi katika maeneo ya Shamsi
yaliyopo jijini hapa.
Alisema siku ya tukio dereva huyo wa
pikipiki akiwa katika eneo hilo
alikuwa anaendesha pikipiki aina ya
Skymark yenye namba za usajili T.
615 BZL huku akiwa amebeba begi
lilionekana kutuna sana, ndipo askari
waliokuwa doria katika eneo hilo
walimtilia shaka na kisha kumfuatilia
na kufanikiwa kumsimamisha.“Mara
baada ya kumsimamisha askari hao
walipekua begi hilo na kukuta silaha
hiyo ikiwa na risasi sita na kisha
kumfikisha mtuhumiwa huyo katika
kituo kikuu cha polisi cha hapa
Arusha mjini”. Alifafanua Kamanda
Sabas.
Kamanda Sabas alisema upelelezi
juu ya tukio hilo bado unaendelea
na mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani pindi utakapokamilika.
Tukio hilo la ukamataji wa bunduki
hiyo limekuja wiki tatu tu baada ya
jeshi hilo kukamata bastola moja
pamoja na risasi 41 kutoka kwa
watuhumiwa waliokuwa
wanahusishwa na matukio ya
kumjeruhi Sister Mary Shobana na
kisha kumnyang’anya fedha taslimu
Tsh 30,000,000/= (Milioni thelathini)
eneo la Notre Dame Njiro lililopo
jijini hapa, fedha ambazo alitoka
kuchukua benki ya Exim tawi la
Shoprite.

No comments:

Post a Comment