Thursday, May 2, 2013

SABABU ZA WATOTO KUFELI HIZI HAPA

Wizara ya elimination kuhamishiwa TAMISEMI.
Watendaji wa Tamisemi badala
ya kusimamia taaluma
mashuleni, wanasumbua na
kuharibu taaluma kwa (a)
kuingilia utawala wa shule
katika kuendesha shule; (b)
kusumbua na kusambalatisha
walimu kila wakati ambapo
wanawakatisha tamaa na
kuwaondolea utashi 'Morale'
wa kufundisha (c) kukata au
kuwanyima mafao yao kwa
makusudi.
2. Wanafunzi kutotimiza
majukumu yao ya kujifunza.
Jamii na wazazi waelewa
kuwaacha tu watoto wao
kuendelea na uzembe.
3. Wanafunzi kutokuwa na
nidhamu mashuleni na jamii
kuwakingia kifua wanapokosa
wasipewe adhabu. Kitu hiki
huhamisha fikra za mwanafunzi
kuwa mtii katika kusoma na
kuwa kichaa na mwenye kibuli.
4. Watoto kuachiwa kutumia simu
mashuleni na maeneo mengine
ambapo muda mwingi
husikiliza muziki, au huchati
na rafiki zake au hupiga simu
za kutongozana na wapenzi
wao. Muda huu ambao ni wa
manufaa kielimu hutumika
isivyo. kwa mwanafunzi kuacha
kusoma na kufikiria kusoma
hawezi kufaulu mtihani.
Mwanafunzi ameweza
kuandika wimbo wa muziki
kwenye mtihani ambayo ni
kazi ngumu ya kutumia akiri
nyingi; kumbe akiri hiyo hiyo
ageihamishia kwenye somo la
kiswahili angeweza kufaulu
hata kama hakuna mwalimu.
wimbo wa muziki ameandika
bila kufundishwa, hata
kiswahili angeweza kujifunza
bila mwalimu kwa kutumia
vitabu na muhitasari.
5. Walimu kutolipwa mishahara
inayoshotosha mahitaji yao
kama wafanyakazi wengine
wenye elimu sawa na wao,
mfano TRA, AFYA N.K. Hii
ingewafanya walimu watulie,
wafanye kazi ya ualimu vizuri
na kuwaza namna ya
kuwaelimisha wanafunzi kwa
matokeo ya kufaulu.
6. Walimu kutotambuliwa na
kuheshimiwa na jamii. Jamii
inawanyanyasa sana walimu
kwa sababu ya msalahi yao
duni. Inafikia mahala baadhi
ya walimu akiulizwa na mtu
ambaye hamufahamu kuwa
anafanya kazi gani, huficha
kazi zao na kutaja kazi zingine
zenye masilahi makubwa ili
kulinda heshima ya utu wake
au ili apatiwe huduma nzuri.
Kitendo cha mwalimu
kutotambuliwa na jamii naye
anaondoa wito wake wa
kufundisha wanafunzi.
Anabakiza tu kuingia darasani
kama muhubiri ambapo
wasikizaji wake hana shinda ya
kuwapima kama wamemwelewa
na yale aliyosema wameyashika
au la. Dawa ni kuwalipa
walimu malipo
yanayowatosha kuishi vizuri.
Mtu fukara katika jamii hana
thamani kwa watu kiushirika
(social life).
7. Ukosefu wa walimu wa
hisabati, sayansi, maabara na
vifaa vya kutosha vya maabara
katika shule nyingi za serikali.
Watoto wawapo shuleni,
wanatakiwa wajifunze mafunzo
yaliyopangwa kujifunza wakati
ule ule uliopangwa kujifunza.
kwa sasa watoto hawajifunzi
wakati ule ule ulipangwa na
wengi hawajifunzi kabisa.
Mwanafunzi anapofanya
mtihani wa somo ambalo
hakufundishwa ipasavyo au
hakufundiwa kabisa, hawazi
kufaulu bali hufeli.
8. Hakuna mtaala wa elimu wa
kudumu unaoeleweka Tanzania
(clear and consistent
curricurum for all Tanzanian
schools). Kwa kuwa mtaala
haueleweki, syllabuses nazo
hazieleweki. kwa kuwa
syllabuses hazieleweki, vitabu
na vitu vingine vya kufundishia
masomo navyo havieleweki.
Mfano: Kwenye somo la
Geography, Mtihani wa mwaka
2012 (csee - SCHOOL
CANDIDATES); swali la 6
ambalo ni la lazima; Mtunga
swali ametumia syllabus ya
1997 hali syllabus iyotumika
kufundishia wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2012
katika shule nyingi za Tanzania
ni ya 2010. Swali linahusu
LEVELLING IN LAND SURVEY .
Topic hii haipo kwenye
syllabus ya 2010 bali ipo
kwenye syllabus ya 1997. Kwa
hali hiyo basi, wanafunzi
walioweza kufanya swali hilo,
ni wale tu waliofundishwa na
mwalimu aliyelitunga na wale
tu waliofundishiwa syllabus ya
1997. Wale wa shule za KATA
na za kawaida hawakuweza
kulifanya, kwa hiyo wakafeli.
Yapo mapungufu mengi sana
ukiyachimbua. CHA KUANDIKA
TU NI KWAMBA, MSIMAMO
IMARA ULIOTULIA WA ELIMU
TANZANIA HAUPO, NA KWA
MAANA HIYO WANAFUNZI
WALIOWENGI HAWAWEZI
KUFAULU HATA KAMA WAKIWA
NA UWEZO MKUBWA KIAKIRI.
MPAKA USANII NA
UBABAISHAJI UONDOLEWE
NDIPO ELIMU TANZANIA
ITAKUWA BORA.
9. Tatizo lingine ni utofauti wa
walimu wanaofundisha
masomo. Mwalimu wa somo
fulani aliyetoka UDSM ni
tofauti na aliyetoka UDOM, ni
tofauti na aliyetoka MWENGE,
ni tofauti na aliyetoka SEKUCO,
ni tofauti na aliyetoka
SOKOINE, ni tofauti na
aliyetoka RUCO, ni tofauti na
aliyetoka ............... Hii ni kwa
sababu hakuna usawazishaji
wa mitaala na course contents
inayofundishiwa katika vyuo
vikuu vya elimu Tanzania.
Matokeo yake ni kwamba
watoto wanakuwa
wanaeleweshwa tofauti tofauti.
Kwa maana hiyo, kwenye
mtihani wa Taifa, wanafunzi
watakaofaulu vizuri ni wale tu
watakaofundishwa na walimu
waliotoka katika chuo kikuu
alichosomea mwalimu mtunga
swali. TANZANIA HAKUNA
MTAALA NA UTARATIBU WA
ELIMU UNAOELEWEKA. Hii
nayo ni mojawapo ya sababu
zilizochamgia wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2012

No comments:

Post a Comment