Saturday, May 4, 2013

Serekali yaanza opereshen kamata makahaba Mrembo brandina awa chambo

MREMBO Brandina Barthon (24),
Jumatatu iliyopita alihukumiwa
kwenda jela miezi 6 baada ya
kupatikana na hatia kwenye kesi ya
ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika
Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji)
jijini Dar.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
William Mutaki ambaye alisema
kutokana na ushahidi uliothibitika,
mahakama hiyo inamhukumu kwenda
jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa
wengine.
Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo
kuchanganyikiwa na kuangua kilio
lakini mheshimiwa hakimu aliamua
kukazia hukumu yake bila ya
kupepesa macho.
Wakati mwanamke huyo akiangua
kilio, afande wa Jeshi la Magereza
alimfikia na kumchukua kwa ajili ya
kumpeleka kwenye Karandinga
kuelekea Gereza la Segerea kuanza
maisha ya jela.
Mbali na Brandina, mwanaume
aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa
mtuhumiwa huyo aliyekuwa
akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga
machozi baada ya kutolewa hukumu
hiyo.

No comments:

Post a Comment