Friday, May 3, 2013

Tambo. Za Baloteli zamponza aachwa na mpenzi wake

MARIO Balotelli ameachwa na
aliyekuwa mchumba Fanny Neguesha
— siku chache baada ya kuripotiwa
kusema kwamba kikosi kizima cha
Real Madrid kingeweza kulala nae
ikiwa wangeitoa Borussia Dortmund.
Mwanamitindo Fanny, 22, aliondoka
kwenye nyumba ya mshambuliaji
huyo huko Italia baada ya
kugombana kutokana kutoelewana
baina ya wawili hao.
Straika huyo wa AC Milan Balotelli,
22, alisema wachezaji wote wa
Madrid
— akiwemo Cristiano Ronaldo —
wangeweza kufanya mapenzi na
demu wake Fanny ikiwa juzi
wangeweza kufanya maajabu ya
kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza
(4-1) na kufanikiwa kwenda
Wembley.
Balo alikaririwa na gazeti la Marca
akisema: “Ikiwa Real Madrid
wataenda kucheza fainali ya
Champions League, nitamtoa
mchumba wangu alale nao wote."
Ingawa baadae alikana kutoa kauli
hiyo.
Balotelli aliachana na mama wa
mtoto wake wa kike mtangazaji wa
TV  Raffaella Fico, 25, kisha ndio
akaanzisha mahusiano na
mwanamitindo Fanny ambaye ana
asili ya Ubelgiji

No comments:

Post a Comment