Monday, May 6, 2013

Raia wa saudia watuhumia kuhusika na bomu arusha

Shabulizi katika kanisa Katoliki la
Arusha la sababisha taharuki
Polisi nchini Tanzania inawashikilia
watu wa nane kwa madai ya
kuhusika na mlipuko wa siku ya
jumapili katika kanisa Katoliki la
Olasit viungani mwa mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao
wako mikononi mwa polisi ni raia
wanne wa Saudi Arabia, na wengine
wanne ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa BBC Baruan
Muhuza akuzungumza akiwa
hospitalini mjini Arusha amesema
idadi ya watu waliofari dunia
kufuatia mlipuko huo ni wawili na
wala sio watatu kama ilivyoripotiwa
hapo awali.
Polisi mjini Arusha vile vile
wamethibitisha kuwa waliokufa
wakati wa tukio hilo la kigaidi ni
wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza
ni kulipuzi aina gani kilitumika
wakati wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye
alitembelea eneo la tukio mbali na
majeruhi hakuna hasara kubwa
iliyotokea mahali hapo pia sakafi na
kuta za kanisa hilo hazikuchimbika
sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad
Mubali anaongezea kuwa watu
wawili sana wamethibitishwa kufariki
dunia katika mlipuko huo uliotokea
majira ya saa tano asubuhi katika
kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya
mji wa Arusha nchini Tanzania na
wengine kadhaa kujeruhiwa huku
balozi wa papa na watawa waliokuwa
katika shughuli hiyo maalumu ya
uzinduzi wa parokia mpya ya
mtakatifu Yosefu mfanyakazi
wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus
Mangwangi ambaye ni paroko
msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la
Arusha mlipuko huo unapotokea
walikuwa tayari katika hatua ya
kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa
kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi
wa Papa Fransis.
Shambulizi la Arusha
Hata hivyo Padre Mangwangi
ameiambia BBC kuwa taarifa
walizonazo muda mfupi baada ya
majeruhi kukimbizwa hospitali watu
kati yao wamefariki huku wengine
wakiendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali ya Mount Meru mjini
Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada
hiyo zimesitishwa huku watalaalamu
wa milipuko na polisi wakiendelea
na uchunguzi kuhusiana na mlipuko
huo.
Bado hakuna taarifa zozote
kuhusiana na chanzo halisi cha
bomu hilo ama kundi lolote
linalodaiwa kuhusika na utegaji wa
bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la
bomu nchini Tanzania japo kuwa
mwaka huu pia kulikuwa na mtukio
ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo
visiwani Zanzibar ambaye alipigwa
risasi wakati akiwa anajiandaa
kuingia kanisani.

No comments:

Post a Comment