Saturday, May 4, 2013

Mfanyabiashara nguli akirusha toka ghorofa ya tisa

TAARIFA za awali zina arifu kuwa
Mfanya Biashara, Costa Shirima
anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya
tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo
Kariakoo Jijini Dar es Salaam
inaelezwa kuwa alifariki dunia muda
mfupi baada ya kujirusha na alikuwa
asafiri na ndege ya saa 10 jioni
kuelekea China kufuata bidhaa za
maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa na
umauti muda mfupi baada ya
kudondoka chini ni mfanyabiashara
aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa
ya urembo wa akina mama yaliyopo
jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka
kwa mmoja wa wanafamilia ambaye
alidai kuwa si msemaji wa familia ya
Shirima ya Mwika Moshi mkoani
Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara
kwamara alikuwa akipendelea kula
katika hoteli hiyo na siku ya tukio
inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa
anapanda juu ya Hoteli hiyo
kupunga upepo baada ya kuhisi
hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda
huko juu ghafla alianguka chini na
kudondokea gari dogo aina ya Toyota
Corola linalofanya biashara ya Taxi
na kupoteza maisha yake na gari hilo
kuharibika vibaya kutokana na
kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa
Mfanya Biashara wa muda mrefu
Kariakoo pia alikuwa akiendelea na
Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya
Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na
watoto 5.

No comments:

Post a Comment