Wednesday, May 1, 2013

Wosia wa lady jay d iwapo atakufa Leo huu apa


maisha yangu nimepitia mambo
mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience
mambo magumu zaidi kadri
ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa
nikipigwa vita sana na watu wenye
uwezo mkubwa kifedha , ki umri
na hata wenye ukubwa wa
connection katika hii industry ya
muziki. Wanaomiliki chombo cha
habari.
Nasimama na kusema kuwa
sitokata tamaa, kwani lengo lao
kubwa ni kuona na kuhakikisha
nimeanguka kabisa na sipo katika
ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa
baridi miaka kumi iliopita, sasa
inazidi kuwa moto baada ya
kutambua kuwa mimi ni mtu
mwenye maamuzi yangu na
misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha
kila mrija unaoniingizia chochote
unakatika, na hiyo ni kutaka
kuuthibitishia umma wa Tanzania
kuwa hakuna msanii anaeweza ku
survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao
mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu
niachane na Tuzo zenu mnazo
influence nani apate nani asipate,
na tangu niachane na Fiesta
nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho
na kuamua kuunda Band ili nijiajiri
na kupata shows zangu mwenyewe,
ikafanikiwa sana jambo ambalo
limewauma na kuamua kufanya
kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote
MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na
kwakuwa watu hao hawanipendi
kabisa, Naamini fika hawataweza
kunipenda hata siku nitakapokuwa
nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu
hao.
Natambua wanaweza kutumia redio
yao kutangaza sana kifo changu na
kusema marehemu alikuwa mtu
mzuri na pengine kupiga nyimbo
zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku
nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo
zangu, wala isiongelee lolote
kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga
wasihudhurie msiba wangu, na
mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na
hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya
kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa
mimi sio ndugu yao, Ila ubaya
wanaoundeleza mioyoni mwao
wanaujua na nina hakika nafsi zao
zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka
mingi na kufanya biashara zangu,
nimekaa kimya watu wanafikiri
nabebwa lakini sijabebwa chochote
sikutaka ugomvi haya mambo
yalianza baada ya Album yangu ya
pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa
Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku
yatakwisha lakini naona moto ndio
unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa
msanii akiwa mkubwa watashindwa
kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki
dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona
hamkuwabeba dada zenu wa tumbo
moja waimbe ili hela irudi
nyumbani??. kama kweli wewe
Kusaga unajua kubeba basi beba
jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza
kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama
mnabisha si mna watoto wabebeni
basi wawe kama kina Diamond ndio
nitaamini kweli nyie mnaweza
kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote
atakaefanya nyimbo na mimi
hazitapigwa, vikao vinne
mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini
endapo wasanii wengine wakiacha
kufanya kazi na mimi?? nyimbo
hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni
nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia
wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo
mmoja nimemsamehe baada ya
kugundua sio hiyari yake ila yuko
under influence ya hawa jamaa
wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke
yake Kusaga ni mfitini kuliko hata
huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi
mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo naomba maoni

No comments:

Post a Comment