Tuesday, May 21, 2013

Kikwete amwagia sifa lowassa


Rais Jakaya Kikwete

amemwagia sifa Waziri Mkuu

wa zamani, Edward Lowassa

hatua ambayo inaweza

kutafsiri mengi katika

medani ya siasa nchini.

Akizungumza na wabunge wa

CCM kwenye Ukumbi wa White

House Dodoma juzi, Rais

Kikwete ambaye pia

mwenyekiti wa chama hicho,

alisema nguvu za Lowassa

pekee zinatosha kushinda

uchaguzi mdogo wa kiti cha

udiwani Kata ya Makuyuni

kilichoko wilayani

Monduli.

Kata ya Makuyuni iko

wilayani Monduli, ambako

Lowassa amekuwa mbunge

wake tangu mwaka 1995.

Habari za kutoka ndani ya

kikao hicho zinaeleza kuwa

Rais Kikwete alitoa kauli

hiyo kuhusu kampeni za

uchaguzi huo wa Makuyuni,

baada ya kuwa ametoa ruksa

kwa makada wa chama hicho

wanaotaka urais kuanza

kujipitisha pitisha

miongoni mwa wanachama wa

chama hicho. Lowassa

anatajwa kuwa miongoni mwa

wanaCCM wanaotaka kumrithi

Rais Kikwete kwenye

Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

“Sina tatizo na pale

Makuyuni, najua muscles

(misuli) za Mzee Lowassa

zinatosha kutupa ushindi;

au vipi mzee?” alidokeza

mmoja wa wabunge wa CCM

akimnukuu Rais Kikwete.

Uchaguzi wa Udiwani Kata

ya Makuyuni unaotarajiwa

kufanyika Juni 16, mwaka

huu, utakuwa wa ushindani

mkali kati ya CCM na

Chadema ambao historia yao

kisiasa mkoani Arusha ni

ya uhasama.

Katika uchaguzi huo,

unaofanyika baada ya kifo

cha Abdillah Warsama

(CCM), chama hicho

kitatetea nafasi yake kwa

kumsimamisha Godluck

Lerunya na Chadema ni

Japhet Sironga. Mbali na

Kata ya Makuyuni, uchaguzi

wa udiwani mkoani Arusha

utafanyika pia katika Kata

za Kaloleni, Themi,

Kimandolu na Elerai,

kutokana na waliokuwa

madiwani wa kata hizo

(Chadema), kufukuzwa na

chama chao.

“Mnaweza kuchafuana leo,

kesho mkapata mgombea

mwenye nundu nyingi na

mabandeji kila mahala,

halafu mkapata shida

kumnadi,” alisema.

Siyo mara ya kwanza kwa

Kikwete kumsifia Lowassa

kwani aliwahi kufanya

hivyo mwaka jana huko

Longido wakati akikabidhi

ng’ombe.

Pia aliwahi kumsifia

wakati wa kampeni za

uchaguzi za mwaka 2010

wakati Kikwete

alipomwelezea Lowassa kama

Mbunge makini na kuwaomba

watu wa Monduli kumchagua

tena.

Hata hivyo, alipoulizwa

kama baada ya kuruhusiwa

kuanza kujipitisha kwa

wanaCCM kama anataka

kuwania urais, Lowassa

alijibu kupitia watu wake

wa karibuni kuwa

asingependa kuzungumzia

suala hilo hasa baada ya

Rais kutoa kauli hiyo.

Kutangaza nia ruksa

Rais Kikwete aliwaeleza

wabunge hao kuwa si kosa

kwa watu kutangaza nia ya

kugombea nafasi mbalimbali

za uongozi ikiwamo urais

mwaka 2015.

“Wabunge na mawaziri wenye

nia ya kutangaza nia ya

kugombea urais wawe huru,

kwani hiyo ni haki yao,

isipokuwa wafanye kwa wema

bila kukivuruga chama na

kuwagawa wanaCCM katika

makundi. Sioni tatizo watu

kujipitisha. Sisi sote

hapa tulijipitisha. Lakini

tufanye hivyo kistaarabu

bila kuvurugana.”'

Aliwaagiza wabunge wa

chama hicho kwenda

majimboni mwao kusikiliza

kero za wananchi badala ya

kusubiri wakati wa

uchaguzi.

Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Kimataifa,

Bernard Membe ambaye naye

anatajwa kuwa miongoni mwa

wagombea amewataka

waandishi waache kuandika

kila siku habari za urais

na badala yake waandike

mambo ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi

wa habari jana baada ya

kukutana na mabalozi wa

nchi zinazoendelea kuhusu

Mkutano wa Smart

Partnership, unaotarajiwa

kufanyika nchini, Membe

alisema ni vizuri

yakaandikwa mambo ya

maendeleo na si kila

wakati kuandika mambo ya

urais.

“Mkutano kama huu nchi

kama Kenya watauripoti

vizuri na kwa undani hivyo

mfanye hivyo si kila kitu

urais 2015,” alisema

Membe. Mkutano huo utaanza

Mei 28, hadi Juni Mosi na

utajadili jinsi gani

sayansi na teknolojia

vinaweza kutumika

kuzikwamua kiuchumi. wa kitaa 

Location : Lema Rd, Moshi,
Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment