Thursday, May 2, 2013

Gadner G naye ajibu mapigo kuhusiana na Wosia wa mkewe

Hivi majuzi lady Jaydee alitoa wosia akidai
kuwa SIKU AKIFA RUGE wa CLOUDS
fm asiguse katika mazishi yake na
Radio Clouds Fm isithubutu
kutangaza wala kutia neno lolote
katika msiba huo……
Gadner G ameamua kuvunja ukimya
na kuufafanua wosia huo kupitia TBC
FM wakati alipohojiwa na mtangazaji
Dan Chibo katika kipindi cha The
Takeover na haya ndo mazungumzo
yao…
————————————
Leo nilipata nafasi ya kuzingumza na
Gadan G Habash ambaye ni Meneja
na Mume wa Mwanamuziki maarufu
nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu
juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay
Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover
kinachorushwa na kituo cha TBC fm
haya ndio yalikuwa majibu ya
maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa
Lady Jay Dee…?
Gadna G: Ni maneno ambayo
yametoka moyoni mwake na ni
maneno mbayo anajitetea kama
msanii, mimi kama Meneja ukiacha
pia kama mke wangu naendelea
kumsapot kwa kile ambacho anaona
ni sawa, basi mimi nitaendelea
kumsaport na kujaribu kuzungumza
na Lady Jay Dee, mara nyingi
anasema tu kwamba watu wasifikilie
ni swala la wimbo kupigwa au
kutokupigwa, hayo ni mambo ya
kawaida lakini wafikirie tu kwamba
huyu mtu anaongea kutokana
experience yake aliyokuwa nayo na
wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha
kufanya kazi kwenye management
yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo
mengi hapa katikati ila hakusema
lakini siku za hivi siku za karibuni
kuna mengine ambayo yametokea,
ndio akaona hapana nisipo sema
nitazidi kukandamizwa na matokeo
yake nitakufa kisabuni.
Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli
swala la kujipanga mara mbili huwa
halipo, ni kwamba unasema ukweli
watu wasikie naukizungumzia
uhasama watu watauliza juu ya
uhasama lakini ulikuwepo tayari
kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa
kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea
lakini tu hawajui tu kwamba jdee
alikuwa na matatizo na wale watu
tangu kipindi cha nyuma sababu
wale watu wanafumo dume ya
kufanya kazi na alipoachananao
aliona kama wanamfatilia kulekule
ambapo yeye alipo
Nini mlikiona kama chokochoko…?
Gadna G: Unajua kwa mfano
unaweza kumuomba mtu maji
akakwambia sina, ukayaona yale pale
ukamwambia niuzie akakuuzia ila
bado alivyokuuzia akaona kama
unafaidi, mwisho akakwambia
yameisha nenda sehemu nyingine,
ukaenda sehemu nyingine na
ukayapata bure, akaona umepata
akaamua kukufata kulekule na
akakukuta unakunywa maji kwenye
grasi kisha akakuputa, sasa hapo
inabidi useme hapa unavyofanya sio
sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee
sasa hivi.
Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani…?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni
kwamba msanii au hata pia stesheni
ya redio inategamea umma wa
Watanzania au hata mashabiki kwa
ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka
Watanzania, basi ujue hata
hajaathirika chochote, na pia tu
anaendelea kufanya kazi kwa bidii,
ila tu isipokuwa unapoona mtu
anafanya madhara ili tu mtu apate
athari fulani ndio unasimama
kuongea, ndiyo maana tuna Bunge
na watu wanasimama, watu
wanaongea, watu wanatetea hoja,
ndiyo maana yake. Yani lazima mtu
usimame useme ukweli kwa unalohisi
hili jambo litanipa madhara
nisiposema.
Kwa Wasanii wengine
unawaambiaje…?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho
binadamu tumeumbiwa, wakati
mwingine unasaidia wakati mwingine
unakudhiru uwoga wako,kwa sababu
wanasema adui wa maendeleo yako
mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo
maana uwoga wako unaeza
ukasabishwa ukakandamizwa zaidi,
ndiyo maana wazee wetu waliweza
kusimama na kuikomboa hii nchi kwa
sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo hii nchi
tusingekuwa huru, kwa hiyo kama
kuna mtu ana jambo na anaogopa
kusema hilo ni jambo la kawaida
kuogopa, lakini wakati wa kusema
ukifika usiogope kusema ili mradi
useme ukweli, basi inatosha….
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji
kujua ukweli na kuambiwa ukweli,
mtu yoyote anayejua kitu cha kweli
anaweza kusema sio sawa,
utaendelea kukandamizwa. Kauli ya
mwisho ndo hiyo wanahitaji
kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili
kama wanakosea wasiendelee
kukosea wabadilikee….
Mwisho..!

No comments:

Post a Comment