Wednesday, May 8, 2013

Form kazi Ipo

MWENYEKITI WA BARAZA LA
MITIHANI NECTA AGOMA KUFUTA
MATOKEO, ASEMA "NITAJIUZULU"
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la
Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu
Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam,Prof.Rwekaza Sympho
Mukandala amesema hayuko tayari
kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.
Chanzo cha karibu cha
Prof.Mukandala kinadai kuwa mara
baada ya kutolewa taarifa ya Serikali
inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha
kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao
na kwa idhini yao.
Iweje leo Baraza libadili
matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya
nani na kwa ustawi wa elimu ya
wapi?' alinukuliwa akihoji
Prof.Mukandala.
Habari za kuaminka zinadai kuwa
Prof.Mukandala pamoja na Katibu
Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako
wanajiandaa kuachia ngazi kama
Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

No comments:

Post a Comment