Monday, May 6, 2013

Babu wa loliondo aendelea kula mafao ya kikombe

Katika kuonesha kuwa Mchungaji
Mstaafu, Ambilikile Mwasapile
‘Babu wa Loliondo’ bado ana fedha
baada ya kuzikusanya kutoka kwa
wateja wake wa huduma ya
kikombe, hivi karibuni alinaswa
ndani ya Benki ya NMB akipata
huduma.
Babu alibambwa ndani ya benki
hiyo Tawi la Loliondo mkoani
Manyara akihudumiwa na mmoja
wa wafanyakazi aliyefahamika kwa
jina la Lembris Lesion ambapo
inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi
ya kujiunga na huduma mpya ya
Jisevie.
Akiwa benki hapo, Babu alionekana
akijaza fomu huku akiwa na begi
ambalo linashukiwa kuwa na fedha
ndani yake ambapo baadhi ya
watu waliokuwa wakimpiga chabo
hawakuonesha kumshangaa
wakiamini bado ana mkwanja wa
kutosha kutokana na ile tiba
ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi
hivi karibuni.
“Unajua Babu alipata pesa nyingi
sana na bado anaendelea
kuzikusanya, kimsingi ana pesa
ndefu benki,” alisema mmoja wa
wateja aliyekuwa eneo hilo

No comments:

Post a Comment