Saturday, May 4, 2013

Mwanafunzi ifm afariki baada ya kulishwa chakula na mpenzi wake ambae ni mke wa mtu

Habari zilizotufikia toka IFM- Dar es
salaam ni kwamba mwanafunzi
mmoja ambaye bado hatujafanikiwa
kulipata jina lake amefariki dunia
kwa kulishwa sumu katika chakula
alicholetewa na mpenzi wake ambaye
ni mke wa mtu……
Taarifa zaidi zinadai kwamba
Mwanafunzi huyo alikuwa na
uhusiano wa karibu sana na mke wa
mtu ambaye mbali na starehe za
kimapenzi alikuwa pia anampekea
chakula cha jioni
Baada ya mchezo huo kudumu kwa
muda, mume wa mwanamke
aliusoma mchezo mzima na kuandaa
tego la kuwaangamiza wote….
Habari zinadai kwamba Siku ya
jumatano jioni mwanaume huyo
aliwahi kurudi nyumbani na
kufanikiwa kukinasa chakula
kilichokuwa kimeandaliwa tayari kwa
kupelekwa kwa huyo mwanafunzi
ambaye alikuwa anatembea na mke
wake…..
Baada ya kukinasa, alijifanya kuzuga
na kupotezea…Mkewe alipotoka
alikichukua na kukitia sumu chakula
hicho na kisha kukiweka kama
kilivyokuwa kimeandaliwa….
Lengo lake lilikuwa ni kuwamaliza
wote maana alijua ni lazima akifika
watakaa na kula pamoja…..
Mwanamke alipopeleka chakula
hakukaa kula na badala yake
alimwambia yule mwanafunzi kuwa
mume wake amewahi kurudi siku
hiyo hivyo hatoweza kukaa wale
pamoja….Mwanafunzi huyo
akakipokea na kukila na ndipo mauti
yakamkuta
Habari toka chuoni hapo zinadai
kwamba mwanafunzi huyo alikuwa
ameshadisco lakini alikuwa amepewa
nafasi nyingine ya kurudia mwaka wa
pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani
kama mwanafunzi….
Mwili wa marehemu bado uko
Muhimbili kwa uchunguzi zaidi
baada ya polisi kuuzuia kuzikwa….
Hizi ni habari mbaya sana kwa
wanafunzi wa chuo hicho maana ni
jumatatu tu mwanafunzi mwingine
alifariki katika hali ya kutatanisha
baada ya kifo cha mpenzi wake miezi
michache iliyopita….
Habari za ndani zaidi zinadai kuwa
toka mwaka huu uanze mpaka sasa
chuo cha IFM kimepoteza wanafunzi
12 huku wawili wakiripotiwa kuwa na
hali mbaya zaidi katika hospitali ya
Muhimbili…. (28)I

No comments:

Post a Comment