Thursday, May 30, 2013
Juhudi za wabunge wa Kenya kuongezewa mshahara zaingia doa
Mahakama nchini Kenya
imesimamisha utekelezaji wa
nyongeza ya mishahara ambayo
wabunge wa nchi hiyo
walipendekeza kujiwekea. Chama
cha mawakili nchini Kenya
kiliwasilisha ombi la kutaka
kuwekewa amri ya kisheria wabunge
hao siku moja baada ya wabunge
hao kupiga kura ya pamoja kutaka
wajoingezee mishahara.
Wanaharakati wamekuwa wakipinga
jaribio hilo huku wakiandaa
maandamano katika barabara za jiji
la Nairobi wakimuomba rais
asiidhinishe kura hiyo.
Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta
aliwafokea wabunge hao kwa uamuzi
wao huku akisema kuwa mishahara
ya wafanyikazi wote wa Umma
inadhibitiwa na tume ya mishahara
iliyoundwa.
Kwa upande wao wabunge hao
wameishutumu tume hiyo wakidai
kuwa ilivuka mpaka wake
kupendekeza wapunguziwe
mishahara yao kwa takriban asili
mia hamsini kutoka dola elfu kumi
kwa mwezi.
Wabunge hao wameelezea hasira
zao juu ya tamko la Rais Uhuru
Kenyatta na tume ya kudhibiti
mishahara ya maafisa wa serikali
ambao wanasema waache vitimbi
vyao vya kutaka kuongezwa
mishahara.
Wanatishia kubadilisha sheria ya
idadi ya maafisa wanaoweza
kuhudumu katika tume za serikali
hadi watatu , kupunguza mishahara
ya maafisa wa serikali kwa asilimia
hamsini na saba na kuwaondolea
wananchi wanaopata chini ya
shilingi elfu hamsini kama ajira
uwezo wa kutozwa kodi.
Wabunge hao hata hivyo hawaoni
ubaya wowote wa kulalamika kuwa
mishahara yao inapunguzwa
wakisema wanasubiri tume ya
bunge kuwalipa mishahara yao ya
laki nane na hamsini kutoka laki
tano
Location : Kisinane Rd, Moshi,
Poudly supported by washari company
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment