Saturday, May 4, 2013

Wolper ajutia historia yake ya mapenzi

DIVA wa kiwango cha juu cha filamu
hapa Bongo, Jacqueline Wolper,
ameonekana kujutia historia yake ya
kimapenzi baada ya kufungukia
kitendo cha yeye kumuanika kila
aliyekuwa akimpenda kwamba
kimemtibulia na sasa amejifunza
kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi
karibuni, Wolper alisema kuwa,
kwenye maisha yake ya huko nyuma
ameshajianika akiwa na wapenzi
tofauti lakini sasa atakayempa nafasi
kwenye moyo wake hatamuanika ila
hilo litakuja baadaye sana kwani
sasa hivi kaweka pembeni kwanza
mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika
maisha yangu ya huko nyuma, hata
hivyo sasa hivi niko bize sana na
kazi, mambo ya wanaume nimeamua
kuyaweka pembeni kwanza,” alisema
Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa
Dallas ambapo kila mtu alijua
alikuwa ni mtu wangu, kwa sasa
nimeamua kutulia kwanza na hata
nikimpata mwingine watu
hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”
Source:Global publisher and antipas

No comments:

Post a Comment