Monday, May 6, 2013

Clouds yajip mapigo yamuasa jide afanye kazi kwa bidii

Baada ya kukaa kimya kwa muda
mrefu, hatimaye mmoja wa
wakurugenzi wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba ameamua
kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi
yake. Ruge amekitumia kipindi cha
Power Break Fast cha Clouds FM,
kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi
Jaydee anavyoendesha harakati zake
na kudai kuwa anapigana kwenye
vita isiyo sahihi.
“Jaydee akaze buti, anapigana na
wrong war, vita yake ameidirect
tofauti na mizinga yake, bunduki
zake amezielekeza kusiko. Skylight
Band inamsumbua, akubaliane na
ukweli kwamba Skylight ndio
iliyoisababishia Nyumbani Lounge
kushuka ilivyoshuka, sio Lady Jaydee
kama msanii.
Vita yake na bunduki zake
azielekezee Skylight
Band.Hajazungumza hata mara moja
kwamba ndio kitu kinachosumbua.
Mimi naamini kabisa akifanya hiyo
kazi, Jaydee bado ni msanii mzuri,
ana nguvu, afanye kazi kubwa ya
kuweza kurudisha mapambano yake
kisanii, kufanya kazi na aangalie
tatizo lililotokea Nyumbani Lounge
labda anaweza akatatua matatizo
lakini sio kushambulia watu kwenye
mitandao,” amesema Ruge.
Hata hivyo amesema yupo tayari
kukaa meza moja na Lady Jaydee
kuzungumza na kumaliza tofauti zao.
“Mimi niko tayari, kesho, kesho
kutwa, kama yupo tayari na ana watu
wengine wengi tu ambao wanahisi
kuna matatizo binafsi ya kuongea na
Clouds, twende sehemu nyingine
neutral tu, tukodishe, tukae pale
tusikie matatizo.
Haisaidii muziki wetu kuonekana
Bongo Flava ni watu ambao kutwa ni
kulalamika, kutwa ni maneno na
matusi tu pale panapokuwa na
matatizo.”
Ameongeza kuwa suala la wasanii wa
Bongo Flava kupenda kutukana
limewafanya hata wasambaji wa
muziki nchini kuacha kufanya kazi
nao.
“GMC kampuni iliyowapa pesa nyingi
wasanii kwenye biashara sio kuwapa
tu kwa kuwagawia, kwa kufanya nao
biashara, sasa hivi huu ni mwaka
wao wa pili na nusu hawajatoa hata
albam moja ya Bongo Flava.
Wasanii wa Bongo Flava wanafikiria
kwa Mamu pamefungwa lakini Mamu
anaendelea na wasanii wa Gospel na
wanauza vile vile.
Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania
akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri
fursa za kiuchumi zinazojitokeza na
sio kupenda kulalamika.
“Turudi kwenye mstari wa kuziona
opportunities, turudi kwenye mstari
wa kusema kwamba leo tunataka
kumzungumzia Jaydee akiwa na
perfume, akiwa na lipstick kama jana
iliyozinduliwa na Rihanna ambayo
nikaambiwa kwamba stock ya lipstick
mpya ya Rihanna iliyozinduliwa
ilikwisha baada ya masaa matatu.
That’s how bigger brand is supposed
to be, and that’s how powerful a
brand is supposed to be katika
namna ya kuunganisha na fursa
zilizopo. Unapokuwa na jina tumia
fursa, tumia opportunities
zinazokuijia wewe kujiendeleza na
kujikuza.
Lakini suala la kulaumiana
halitatukuza kwasababu sisi ni radio
binafsi, tutafanya kile tunachokifanya
sisi kwa matakwa ya wasikilizaji wetu
wengi zaidi, tukiiangalia faida kama
motivation, tukiiangalia social
responsibility kama motivation yetu
ya pili, in the long run kuangalia
tunakotaka kwenda kufikia strategy
ambayo kampuni yetu inajiwekea.”
Ruge pia amewakumbusha wasanii
kutojisahau kwakuwa hakuna msanii
anayeweza kuhit maisha yake yote.
“Tuwaandae wasijisahau, na katika
hili simzungumzii Jaydee peke yake,
nazungumzia wasanii wote wa
Tanzania nawazungumzia kuelewa
kwamba tunajisahau sana.
Tunapata hela nyingi sana,
sitashangaa miaka mitatu baada ya
leo, Ommy Dimpoz naye ukamsikia
anaandika hivi hivi, au Diamond
naye ni kwasababu hakujipanga tu.”
Kuhusu shutuma kuwa Clouds FM
inaua muziki wa Bongo Flava, Ruge
amesema, “inanishangaza kidogo
kwasababu Clouds inategemea
matangazo ya biashara kwa asilimia
95, ndio biashara yake hiyo.
Lakini inategemea muziki wa Bongo
Flava kama maudhui ya kipindi,
inaanzaje kuuua, inategema wasanii
wa Bongo Flava kama wasanii wa
kwenda kufanya shows mkoani.”
Kuhusu msimamo wa kampuni Ruge
amesema:
Msimamo wa kampuni ni kwamba
tunaamini kabisa mwanadada kinara
wa muziki wa Tanzania naamini
atakaa na kutafakari la kufanya.
Tunamtakia kila lakheri kwenye show
yake ya tarehe 31 afanye vizuri lakini
atakapokuwa tayari sisi tuko tayari
kuendelea kufanya kazi, anajua cha
kufanya.

No comments:

Post a Comment