Wednesday, May 1, 2013

Wamewauwa watu lakn kesi yao mizengwe tu mafisadi bhana

Kesi ya mv islander yashidwa kufanyika washitakiwa katika kesi hiyo ni Said
Abdallah Kinganyiti (58), Abdalla
Mohamed Ali (30), Yusuf Sleiman
Issa (47), Haji Vuai Usi (53), Abdalla
Moh’d Abdalla (46), Juma Seif Juma
(55),
Hassan Mussa Mwinyi (50), Shaibu
Said Mohammed (39), Salim Said
Mohammed (37), Makame Hasnuu
Makame na Jaku Hashim Ayoub.

Zanzibar: Upande wa mashitaka wa
Serikali umeshindwa kuwasilisha hati
za hatua ya awali ya usikilizwaji wa
kesi ya meli ya MV Spice Islanders
iliyozama na kuua mamia ya watu
Zanzibar na kuiomba Mahakama Kuu
iwape muda zaidi.
Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)
Zanzibar, Omar Sururu alidai jana
kuwa katika hati hiyo wameona bado
kuna upungufu ambao unaweza
kuleta matatizo wakati kesi
ikiendelea na kuomba wapewe wiki
mbili.
Wakili wa upande wa utetezi,
Abdalla Juma alipinga ombi hilo na
kudai kwamba upande wa mshitaka
ulipewa muda wa kutosha wa
kuwasilisha hati hiyo.
Wakili huyo aliomba kesi hiyo
isikilizwe,kwani washtakiwa baadhi
yao wamesimamishwa kazi kwa hiyo
inawapa athari kubwa.
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman
Makungu anayesikiliza kesi hiyo
aliutaka upande wa mashtaka
kuwasilisha hati hiyo Mei 13 mwaka
huu na kesi hiyo itatajwa Mei 16
mwaka huu.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Said
Abdallah Kinganyiti (58), Abdalla
Mohamed Ali (30), Yusuf Sleiman
Issa (47), Haji Vuai Usi (53), Abdalla
Moh’d Abdalla (46), Juma Seif Juma
(55),
Hassan Mussa Mwinyi (50), Shaibu
Said Mohammed (39), Salim Said
Mohammed (37), Makame Hasnuu
Makame na Jaku Hashim Ayoub.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na
mashitaka ya kuua bila kukusudia
kinyume na kifungu cha 195 na 198
cha sheria namba 6 ya mwaka 2004
ya sheria za Zanzibar.
Meli hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka
Unguja kwenda Pemba ikiwa
imebeba abiria 2,470 ilizama Nungwi
katikati ya mkondo wa bahari usiku
wa Septemba 9,2011 na watu 941
walinusurika katika ajali hiyo.KAMA SI UFISADI NI NINI NAKARIBISHA NAOMI

No comments:

Post a Comment